
Kampeni
inayoaminika kuanzishwa na mashabiki wa Wema Sepetu ikiwa na hash tag
#BringBackOurWema wakimtuhumu Diamond kuwa chanzo cha muigizaji huyo wa
kike kushuka ngazi kwenye tasnia ya filamu.
Sauti
za mashabiki hao imemfikia vyema Diamond Platinumz na amemua kujibu
mashambulizi kwa kuandika ya moyoni kuhusu mpenzi wake huyo akidai kuwa
yeye mwenyewe ndiye chanzo cha tatizo kwa kuwa ameendekeza maisha ya
anasa na mashoga wanaompoteza.
“Nafikiri
ningewaona kweli mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa wasanii wenu….kama
mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na
Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta
maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…Mimi kama bwana, wajibu
wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala
vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi Waswahili wanasema
Mchungaji bora anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa
mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie???? Nisiende
Studio nikae dukani nimuuzie mie???? Ni juhudi zako kwanza!...leo hii
mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo mie
mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu
nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeew! Kama nimekuchagua Lamba ndimu
usitapike.”
Post a Comment