Acha kabisa! Habari ya
mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva,
Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa
wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money.
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akipozi kimahaba na Vanessa Mdee, 'V-Money'.“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema:
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akishow love na Jokate Mwengelo ‘Kidoti’.Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.
Post a Comment