Watoto watatu wadogo waliobakwa kwa zamu na watoto wenzao.
Wazazi wa kiume wa watoto hao.
Wakizungumza na gazeti hili kwa masikitiko kwa nyakati tofauti,
wazazi wa watoto hao walidai kwamba walipowabana waliwataja kwa majina
waliowafanyia vitendo hivyo, jambo lililowafanya ‘kuwataiti’ watuhumiwa
kwani walikuwa wakiwafahamu.Wazazi hao walidai kwamba walipowauliza watoto hao walikiri kuwaingilia wenzao kwa zamu kwenye jumba bovu (pagala) ambapo walienda mbali zaidi na kusema kuwa walikuwa wamewafanyia vitendo hivyo kwa muda mrefu sasa kwa zamu, nyakati ambazo watoto hao walirejea kutoka shuleni chekechea (jina kapuni kimaadili).

Wazazi wakike wa watoto hao.
“Nilishtuka na kuumia sana baada ya kugundua mwanangu ameingiliwa, tena kwa kipindi kirefu kiasi kwamba ameharibika kabisa.“Huwezi kuamini mke wangu alipopata taarifa alipandwa na presha kiasi cha maisha yake kuwa hatarini,” alisema mmoja wa wazazi hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Hussein.

Walaka wa polisi wa kukamatwa kwa watuhumiwa.
Kwa pamoja wazazi hao waliripoti ishu hiyo kwenye Kituo cha Polisi
cha Charambe na baadaye Mbagala-Kizuiani ambapo majalada ya kesi hizo
yalisomeka MBL/RB/9608/14-KUBAKA, CHAR/RB/1292/2014-KUBAKA CHAR/RB/2192/2014-KUBAKA ambapo watuhumiwa wanasubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Post a Comment