Mshiriki
wa filamu mpya ya Fundi Seremala, Kajala Masanja ameanza
kumfichua mpenzi wake mpya baada ya kuingiza mtandaoni picha
inayomuonyesha akipigana mabusu na kijana mmoja ambaye
hakujulikana jina lake mara moja, anayehisiwa kuwa mpenzi mpya
wa mwigizaji huyo…..

Kajala
ambaye katika filam ya Fundi Seremala ameigiza kama mmoja wa
washiriki wakuu anadaiwa kuziachia kwa makusudi picha hizo ili
kuuondoa uvumi wa kumzunguka aliyekuwa rafiki yake Wema Sepetu
na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake,
Clement.

Hata
hivyo, Kajala bado hajasema lolote kuhusiana na picha hizo
licha ya picha hizo kusambaa kwa kasi katika mitandao ya
kijamii
Post a Comment