Keyshia
Cole ambaye hivi karibuni amepigana chini na mume wake Daniel
Gibson ‘Boobie’, mwishoni mwa wiki jana aliachia video yake mpya
ya wimbo wa She, ambayo ilishangaza wengi kutokana na kuwamo
matukio ya muonekano wa kushabikia mahusiano ya kimapenzi ya
jinsia moja ( Usagaji )

Katika
video hiyo, Keyshia Cole anaonekana akimchezea kimahaba msichana
mwenzake anayeonekana kufanana naye kwa sura, huku wakiwa
chumbani, jambo lilioonekana kama kuashiria aina yake mpya ya
mahusiano ya kimapenzi hasa kutokana na kuachana na mumewe
siku chache zilizopita….
Hata
hivyo, Keyshia Cole amejitetea kuwa wimbo huo uliotayarishwa na
DJ Mustard hauhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanamke na
mwanamke.

“Ni wimbo wa kimapenzi, lakini hauhusu mapenzi ya mwanamke na mwanamke kama inavyodhaniwa,” amejitetea Keyshia Cole
Post a Comment